top of page
Search

Idrisa Mchilowa Amri ni Mpatanishi wa Huduma za Afya na Jamii Mtwara.

  • Writer: Idrisa Mchilowa Amri
    Idrisa Mchilowa Amri
  • Jul 5, 2024
  • 2 min read


Mimi Idrisa Mchilowa Amri ni mkazi mkoa wa Mtwara katika Halmashauri ya Mtwara Mikindani, Ni mmoja wapo ya wanufaika Wa Kijana na Afya Bora (Youth Champion For Global Financing Facility) ambapo Mtwara ni miongoni mwa maeneo ambayo mradi umefanya utekelezaji.


Wakati wa Mafunzo

Kwenye haya mafunzo nimepata kutoka na ushiriki kwa namna zote wakati wa mafunzo kwa kipindi chote pia kwenye upande wa menejimenti ya utekelezaji maendeleo na mafunzo yalikua ni mazuri. Ningependa kueleza namna sahihi ya kuwajibika kwenye swala la afya katika jamii nikiwa kama kijana na mnufaika wa mradi huu kwa kufuata miongozo kama vile katiba Ya Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania katika swala zima la haki ya afya bora kwa kila mtanzania.. 


Wajibu wa jamii

Jamii Inatakiwa kuwajibika kwa kufuata mbinu au njia kwenye ushiriki na kwenye uelewa kuhusu afya pia kujua kuwa kwenye uwajibikaji tuzingatie upataji sahihi wa taarifa, kuunda vikundi Kazi vitakavyowezesha ushiriki. Nilichopenda Ni Vile mafunzo yametambua Uhitaji /Nini Jamii Inahitaji Kwa upande Kutambua Wajibu Wao Kama Jamii, Afya ,Elimu ,Itakavyo Wapelekea Kuishi salama na amani katika jamii zao. 


Matarajio yangu

Matarajio kwa Kile nilicho jifunza nitakuwa balozi na mwakilishi mzuri katika kutoa elimu katika jamii, kwa sababu Kuwapa elimu mafunzo Kwa kuwashirikisha nitakuwa Kitu Kimoja Wataelimika Kwa Kufuata Na kuishi kwa Afya Bora.


Habari kutoka field Mtwara

1.Jamii /Umma Kwa Kutumia Chombo husika kuungana kulitokana na kuulizwa Maswali Kwa Vijana juu ya maswala mbali mbali ya afya ya uzazi.

2. Wakina mama ambao Wanapokea /Kupata huduma za afya kwenye kituo na nilipata uelewa wa maarifa kwa kile walicho kuwa wanauliza Kuhusu Afya Ya Uzazi

3. Kuwajibibika kwa namna ya kufahamu upatikanaji wa taarifa sahihi na kuwekeza katika kujifunza

4. Ushirikiano mzuri kati ya jamii na vituo vya afya vilivyo karibu na wao.


Kituo cha Afya Likombe ni kituo bora,maboresho ni kidogo tu.


Uelewa wangu kwenye kituo cha afya ni kuwa hakuna upendeleo wala uonevu wowote kwa makundi yote. Pia nilipenda vipaumbele vitolewavyo kwa Wazee na kwa kina Mama Na Wajawazito hadi muda mwingine wasiokuwa na uwezo na kugharamia.  Upatikanaji wa dawa ni toshelevu pia

Kupitia Community Score Cards ilikuwa kama chombo /kifaa cha kuwajibika katika Jamii. Tulishiriki kwenye jamii na wahudumu wa afya ,Kamati za afya katika kituo cha afya Likombe kilichopo manispa ya Mtwara Mikindani na tuliweza kuelimisha jamii ambayo kwa sasa inafahamu juu ya afya bora na kiwango cha kukuza nguvu kazi kwa Taifa. 


Shukrani za dhati kwa Serikali kupitia Ofisi ya Raisi TAMISEMI pamoja na Wizara ya Afya kwa kutupa vibali na ushirikiano kutekeleza majukumu haya. Shukrani pia kwa Young and Alive Initiative pamoja na wawezeshaji wa programu hii Population Action International(PAI). Makala ijayo itaelezea zaidi maendeleo ya kazi hii Mtwara.


" Jamii Imara ni lazima iwe na mahusiano chanya na kituo cha afya karibu na hiyo jamii husika" Rajab Mchilowa Amri kutoka Mtwara

 
 
 

Comentários


bottom of page