top of page
Search
  • Rajab Hunge

Rajab wa Chuno ni kama Canvas!!

Kwa jina ni Rajab Hunge, Afisa tabibu na msanii (poet & storyteller). Imekuwa fahari kwangu kuwa miongoni mwa vijana waliochaguliwa kama champions na kushiliki fellowship ( YAI Champions fellowship 2023/24) hii kama ilivyo kusudiwa.

Wakati wa mafunzo

Awali nilipokuwa najiunga kwa kuanza kama mshiriki nilikuwa mfano wa ‘canvas’ isiyo na maandishi au mchoro juu yake, kwa maana ya kuwa haikuwa na thamani ambayo mtu angejifunza kutokana nayo chochote zaidi ya kuishangaa na kutaka kuipakaa rangi hovyo au kuichora chochote ikiwa kama mtu angepewa. Ndiyo, kuichora kwa maana ya kuwasilisha hisia kwa sanaa au kuhifadhi maarifa fulani juu yake, naamini hali hiyo ya mimi kuwa tupu mfano wa canvas imekuwa ni nafasi kubwa kwangu kupokea michoro na rangi bora kutoka kwa wachoraji (waalimu), nayo ni maarifa na taarifa ambazo zimejenga ujuzi kutokana na mradi, Naweza kusema ‘canvas si canvas tena’ bali ni mchoro maaana wasanii wametia mikono yao na wakaipendezesha kwa brushes na rangi kwa kuwasilisha walichokusudia. Haikuwa kwa siku moja, ukuaji na mabadiliko yamekuwa ya kitokea kidogo kidogo mpaka kufikia kiwango cha kudhihirika na kutumika hii inatokana na athari ya maelekezo kutoka kwa waalimu ambayo yamekuwa yakinijenga na kunipatia uelewa wa mradi na taarifa za msingi ambazo zimekua sehemu ya kuongeza maarifa binafsi na utekelezaji wa mradi pia.


Katika hatua ya mwanzo ya mafunzo ya mradi nimenufaika kwa kujifunza masomo ya, uadilifu, nadharia na misingi ya uongozi wa kijana katika ubinafsi wake na pia katika jamii hususani katika masuala ya afya, uwajibikaji jamii, uchechemuzi na ufuatiliaji kama namna ya kuchochea mabadiliko chanya katika uboreshaji wa huduma rafiki za uzazi na lishe kwa vijana kwenye jamii zao. Katika kujifunza nilipendezwa na namna ya uwasilishwaji wa mada kutoka kwa walimu kwa kufanya marejeo na kutupa picha ya matumizi halisi ya taarifa na maarifa hayo katika maisha yetu binafsi na jamii zetu pia hii ni kuanzia uongozi bora, uwajibikaji na uchechemuzi katika ya masuala afya ya uzazi katika jamii lengwa.


Aidha katika kuboresha zaidi namna ya utoaji wa mafunzo ya awali ya mradi ni kwa kuweka mazingatio ya namna ya ufanyaji wa mafunzo kuanziaa urahisi wa matumizi ya mitandao kwa waalimu na wanafunzi kwa kuzingatia muda lakini pia kupata uzoefu wa uwasilishaji wa masomo katika namna ya kuokoa muda badala ya kutumia muda mwingi sababu ya ugumu wa uwasilishaji wa somo wakati wa kipindi.


Utekelezaji wa mradi


Japokuwa mimi si mkazi wa eneo ambalo lilikuwa chaguo kwa kutumika kama sampuli ya utekelezaji wa mradi (Chuno), bado hilo halikuzuia utekelezaji wa zoezi hilo huku wengi katika wanajamii waliohusishwa wakionyeasha ushirikiano wa kuridhisha katika kutoa taarifa na mawazo kadri ya muongozo wa mjadala ambao ulikuwa wa namna ya mazungumzo ya majibizano (dayalojia).


Ikiwa kama sehemu ya utekelezaji wa mradi kwa  vitendo, mwezi Aprili 2024, katika mkoa wa Mtwara (Mikindani) nilifanikiwa kulitekeleza hilo kwa msaada wa timu na viongozi wa mradi na kukutana na wanajamii ambao walikuwa ndio watahiniwa wakuu kwa muongozo wa mijadaala huru na dodoso lililo andaliwa likipima kiwango cha uelewa wa afya ya uzazi na kuangazia  upimaji wa uwajibikaji wa wahusika wa utoaji wa huduma za afya katika kituo kwa kuwa shirikisha wanawake (akina mama), wanaume  na vijana ambao ni wateja wa kituo nilichokitumia kama sehemu ya uekelezaji wa mradi (Chuno dispensary). Aidha katika kupima uwajibikaji nilishirikisha viongozi wa kata na kamati ya afya ya Kijiji na mwisho kufanya tathmini ya utoaji wa huduma kwa kuwahusisha watoa huduma na kuhitimisha kwa kupima ukamilifu wa miundombinu ya kituo (zahanati) kwa kurejea miongozo ya wizara ya Afya.


Shukrani za dhati kwa Serikali kupitia Ofisi ya Raisi TAMISEMI pamoja na Wizara ya Afya kwa kutupa vibali na ushirikiano kutekeleza majukumu haya. Shukrani pia kwa Young and Alive Initiative pamoja na wawezeshaji wa programu hii Population Action International(PAI). Makala ijayo itaelezea zaidi maendeleo ya kazi hii Mtwara.


Mimi ni Rajab Hunge Afisa Tabibu na Msanii wa hadithi na mashairi.

73 views0 comments

留言


bottom of page